, Bosi wa simiti ya Rai apatikana amekufa, miguu na mikono kufungwa

Bosi wa simiti ya Rai Chetan Vyas Jumanne alipatikana amekufa katika kaunti ya Kericho.

Mwili hiyo iligunduliwa ndani ya chumba chake cha kulala nyumbani kwake kilicho ndani ya majengo ya kiwanda katika Sigowet  kata ndogo ya Soin.

Kamanda wa Polisi wa Kericho Paul Nasio alifichua kwamba watuhumiwa walipata kuingia chumbani kwake kupitia paa la nyumba hilo.

“Waliinua mabati kutoka paa, na wakapata kuingia kwa nyumba kupitia stoo la jikoni kabla ya kuelekea chumbani ambapo Siaz alikuwa amelala,” aliiambia Citizen Digital.

, Bosi wa simiti ya Rai apatikana amekufa, miguu na mikono kufungwa
Chetan alikuwa meneja wa simiti ya Rai

Mikono na miguu yake ilikuwa imefungwa kwa kamba ambayo pia ilikuwa imefungwa shingoni.

Naibu kamanda wa polisi wa Kericho pia alisema watuhumiwa waliitenga kamera ya nje ya CCTV lakini picha zao zilikamatwa ndani ya nyumba hiyo.

Walakini, haikuwezekana kuwatambua kwani walikuwa wamevaa vifaa vya kuficha uso wakati huo.

Bosi wa polisi alibaini zaidi kwamba majambazi walitokomea na mifuko kadhaa ambayo haijulikani ni nini iliyomo ndani.

Source link